Bila shaka wale waliokuwa wakiponda usajili wa kiungo mshambuliaji Clatous Chama kutua Yanga mpaka sasa wameanza kupata majibu kwa nini Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alihakikisha Mwamba huyo wa Lusaka anaitumikia Yanga msimu huu
Chama alianza taratibu lakini mechi hadi mechi ameendelea kuonyesha kwa kiasi gani Yanga ilimuhitaji katika kikosi chake msimu huu ambao Wananchi wanalenga kufanya vizuri zaidi katika ligi ya mabingwa
Chama ameendelea kuweka rekodi katika michuano hiyo baada ya jana kufunga bao lake la 20 katika ushindi wa mabao 6-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Vital'o
Aidha katika mchezo huo, Chama alihusika katika mabao matano kwani licha ya kufunga pia alitoa pasi nne za mabao
Katika mechi zote mbili dhidi ya Vital'o, Chama amehusika katika mabao 7 akifunga mawili na kutoa assist 5
Sasa anashika nafasi ya sita barani Afrika katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa kwa muda wote. Ana mabao 20 mguuni mwake na assist 12
Katika mechi tatu zilizopita, Chama amehusika katika mabao nane, amefunga mawili na kutoa assist 6