Washambuliaji wa Yanga ambao ni majeruhi Donald Ngoma na Amissi Tambwe wamewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa na umoja wakati huu msimu wa ligi kuu ya Vodacom ukielekea ukingoni.
Wakizungumza katika kipindi cha Yanga TV kilichoanza kuruka leo Ijumaa kwenye runinga ya Azam, wachezaji hao pia wamefunguka kuhusu majeruhi yao.
Ngoma amekanusha uvumi unaosambazwa kuwa amegoma kucheza bali akathibitisha kuendelea kuuguza majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa miezi saba sasa.
Ngoma amewataka mashabiki wa Yanga kuwa na uvumilivu juu yake pia kumuunga mkono katika kipindi hiki kigumu anachopitia.

Naye Amissi Tambwe amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa kuendelea kuwa nae bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu anachopitia.
Tambwe amesema alitonesha jeraha la goti wakati akiwa katika mazoezi ya klabu ya Yanga mkoani Morogoro.
Ameushukuru uongozi wa Yanga kwa kuendelea kuwahudumia vyema licha ya kuwa nje kwa muda mrefu.
"Najua wote mnafahamu mimi nkiwa mzima huwa nafanya vizuri, kwa sasa ninapitia wakati mgumu. Nashukuru viongozi wameendelea kutusaidia."

ADVERTISE HERE