Mzize yuko mikononi salama Yanga - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Aug 2024
Mzize yuko mikononi salama Yanga - Hersi

Licha ya ofa kutoka klabu ya Wydad Athletic, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameweka wazi msimamo wa klabu juu ya mshambuliaji Clement Mzize

Hersi amesema hayatakuwa maamuzi sahihi kwa klabu kumruhusu Mzize akajiunge na Wydad klabu ambayo kwa sasa 'inajitafuta' baada ya kupoteza makali yake

Hersi amesema Mzize anapata kila kitu Yanga na kwa sasa sio wakati sahihi kwake kuondoka

"Kuna timu nyingi sana ambazo zimeleta ofa kwa wachezaji wetu hata hii timu ambayo ndo kwanza inajijenga (Wydad) walileta ofa ya kumtaka Mzize

"Lakini ukiingalia ndo kwanza wanajijenga hivyo kwa maoni yangu sio sehemu ya Mzize kwenda kucheza, tunampelekaje kwenye timu ambayo haichezi klabu bingwa?"

"Yanga ina kila kitu ambacho mchezaji anahitaji anakipata kwa hiyo tunapomtoa mchezaji lazima aende kwenye timu kubwa zaidi yetu," alisema Hersi

Wydad waliwasilisha ofa yenye thamani takribani Milioni 270 ambayo ingeweza kufika Milioni 400 lakini uongozi wa Yanga ukasisitiza kama wanamtaka basi wafuate masharti ya mkataba wake ambao una kipengele cha kumnunua kwa Tsh 2.7B

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’