Yanga itampa Gamondi heshima Afrika - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2024
Yanga itampa Gamondi heshima Afrika - Hersi

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amefichua haikuwa rahisi kumbakisha kocha Migue Gamondi baada ya mafanikio aliyopata msimu uliopita

Akizungumza katika mahojiano maalum ndani ya kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi Fm, Hersi alisema Gamondi alipata ofa nyingi lakini baadae aliamua kubaki Yanga kutokana na ubora wa kikosi alichokijenga

"Kabla ya kusaini mkataba mpya, Kocha wetu Miguel Gamondi alipata ofa nyingi sana kutoka Klabu nyingine kubwa Afrika na aliahidiwa hela nyingi"

"Lakini alichagua kubaki Yanga kwa sababu ya ubora wa timu tuliyoitengeneza. Hii timu yetu inaweza kumpa heshima kubwa zaidi Afrika," alisema Hersi

Hersi amesema katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, Yanga imeweka malengo ya kufika robo fainali kama walivyofanya msimu uliopita hata hivyo amesema kama watafanikiwa zaidi ya hapo basi itakuwa zawadi kutoka kwa Mwenye ez Mungu

"Malengo yetu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu ni tufike tena hatua ya robo fainali. Lakini kwenye maisha M/Mungu hutoa zawadi, tukipata zawadi ya kufika Fainali na kuchukua Ubingwa basi tutashukuru. Target yetu ni Robo Fainali na tutapambana kufanikisha hilo"

Katika hatua nyingine Injinia Hersi amemshukuru Mdhamini/Mfadhili wa Yanga GSM kwa sapoti yake kila hatua akiwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kumshukuru na kumuombea bilionea huyo kwa upando wake kwa klabu

"Kama kuna jambo ambalo Wanayanga wanapaswa kuliombea dua liendelee ni uwepo wa GSM kwenye timu yetu, amekuwa akitusapoti katika mambo mengi mno"

"Mfano juzi kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuwashughulikia watu fulani, alikuja na kutuuliza bajeti ya bonasi ikoje, tulipomwambia akasema haitoshi, akaongeza fungu la maana vijana wakaenda kupambana tukashinda" alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’