Klabu ya Wydad Athletic imewasilisha ofa kwa Yanga ili kumsajili mshambuliaji kinda wa timu hiyo Clement Mzize, imefahamika
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imethibitisha kuwa Wydad wamewasilisha ofa yao ya kwanza ambayo hata hivyo imekataliwa kwa sababu haijafikia thamani halisi ya mchezaji
Yanga wamegoma kupokea takribani Tsh Milioni 270 (dola 100,000) huku wakiweka msimamo wa kuhitaji takribani Bil 2.7 kumuachia Mzize ambaye aliibuliwa katika kikosi cha Yanga U20 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa miwili iliyopita
Mzize ni miongoni mwa washambuliaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu huu, haitakuwa rahisi kwa Wananchi kumuachia akaondoka kwa dau dogo
Kocha Mkuu wa Wydad Athletic Rulani Mokoena alimuona Mzize katika mechi za ligi ya mabingwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi zote mbili dhidi ya Mamelodi Sundowns iliyokuwa ikinolewa na Mokoena wakati huo
Baada ya jitihada za kumnasa Stephane Aziz Ki kukwama, Mokoena amerejea tena Jangwani kwa nguvu kubwa sasa akitua kwa Mzize