Msimu huu Yanga imekuja na sera tofauti kwa timu yakeya vijana ambapo unafanyika usajili wa kimkakati ili kuhakikisha timu hiyo inakuwa na ushindani
Lengo ni kuona klabu inaanza kunufaika na timu za vijana moja kwa moja kwa kuwapandisha wachezaji timu ya wakubwa au kuwauza
Nyota kadhaa wa Yanga U20 wametolewa kwa mkopo ili kuwaimarisha zaidi huku nyota wengine wakisajiliwa
Moja ya sajili bora zilizofanywa ni kiungo mshambuliaji Omar Mohsin akitokea Dar es Salaam Soccer Academy
Mohsin ni mmoja wa nyota wanaokuja vyema ambapo mchezaji huyo alipata mwaliko wa kufanya mazoezi na Spain Rush Academy huko Hispania hivi karibuni
Yanga imepanga kumjumuisha katika kikosi cha kwanza lakini ataanzia na timu ya vijana
ADVERTISE HERE