Wachezaji Chadrack Boka na Jean Baleke jana hawakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoikabili Vital'o katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika
Sababu ya nyota hao kutotumika ziliwekwa wazi mapema, kuwa ITC zao zilichelewa ambapo Yanga ilizipokea wakati tayari dirisha la usajili la CAF likiwa limefungwa
Nyota hao walisajiliwa kwa ajili ya kutumika katika ligi ya mabingwa pia lakini kwa kuwa ITC hazikufika kwa wakati wamezuiwa kushiriki mechi mbili za hatua ya awali
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa wachezaji hao watakosa mchezo wa marudiano dhidi ya Vital'o utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki ijayo lakini watakuwa sehemu ya kikosi katika mechi zitakazofuata kama Yanga itafuzu
Kwa maana watashiriki mechi ya raundi ya kwanza dhidi ya Sc Villa/CBE Ethiopia