Ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga wameupata dhidi ya Vital'o leo una maana kubwa kwa Wananchi
Kwanza Yanga imejiweka katika nafas nzuri ya kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kimahesabu Yanga inahitaji sare katika mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki ijayo
Lakini pia Wananchi leo wamekusanya Tsh Milioni 20 ambayo ni bonasi ya goli la Mama
Kama ilivyokuwa misimu iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. Samia Suluhu Hassan anaendelea kutoa bonasi kwa kila goli katika mechi za Kimataifa ambazo matokeo yake ni ushindi kwa timu ya Tanzania


ADVERTISE HERE