Dirisha la usajili lililofunguliwa Juni 15, linatarajiwa kufungwa leo Alhamisi August 15, saa 5:59 usiku
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu kukamilisha usajili ndani ya muda ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi
Katika dirisha hili Yanga imesajili wachezaji saba ambao ni mlinda lango Aboubakary Khomein, mlinzi Chadrack Boka, viungo Aziz Andambwile, Clatous Chama na Duke Abuya pamoja na washambuliaji Jean Baleke na Prince Dube
Yanga huenda ikafunga usajili kwa kuongeza beki mwingine wa kati ambaye ni wa ndani
ADVERTISE HERE