Tutamaliza mechi dhidi ya Vital'o Azam Complex - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2024
Tutamaliza mechi dhidi ya Vital'o Azam Complex - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex siku ya Jumamosi katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Vital'o ya Burundi

Kamwe amesema wanataka kuitumia mechi ya Jumamosi kukata tiketi ya kutinga raundi ya kwanza kwani katika mechi ya marudiano watafanya sherehe kubwa ya kukaribisha msimu katika uwanja wa Benjamin Mkapa

"Tumepata bahati wapinzani wetu Vital'o wamechagua kutumia uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani. Hivyo Jumamosi sisi tutakuwa ugenini Azam Complex na mechi yetu ya nyumbani itapigwa August 24 katika uwanja wa Benjamin Mkapa"

"Nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Azam Complex kwani huu ndio mchezo wa kutupeleka hatua inayofuata katika michuano hii"

"Mechi yetu itakayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa tutaitumia kama sherehe ya kukaribisha msimu mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa," alitamba Kamwe

Baada ya kutwaa Ngao ya Jamii, Yanga ilirejea mazoezini juzi kujiandaa na mchezo huo ambapo jana ilicheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Green Worries na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Avic Town

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’