Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amewashukuru mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa ushirikiano na sapoti wanayoitoa kwa wachezaji wao katika kuhakikisha timu nafikia malengo yake
Jana Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Pacome amesema mashabiki wa Yanga wamekuwa chachu kwa wachezaji kufanya vizuri akiwataka Wananchi kuendeleza utaratibu huo wakati wakielekea kwenye michuano ya ligi ya mabinwa ambayo msimu huu wameweka malengo makubwa
"Nichukue nafasi hii kuwashukuru Wananchi kwa sapoti yenu usioyumba, maana siku zote mmekuwa pale kwa hali yoyote ile ili kutusukuma kupata ushindi"
"Asante na hongera sana kwa Kombe la jana, nasema sisi, kwa sababu. tunashinda na kushindwa pamoja! Na ni wakati wa kuwaambia kwamba tutapambana kwa msimu ujao na hasa kwa kipaumbele chetu kikubwa ambacho ni Ligi ya Mabingwa"
"Tutapambana katika kila namna lakini ili kufikia hili tunahitaji mtu wetu wa 12 ambaye si mwingine bali nyinyi wananchi. Tunaahidi kuwafanya muwe na furaha msimu huu kwa sababu tuna malengo yaliyo wazi" Asante na msimu uanze," aliandika Pacome katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Pacome amerejea akiwa 'fit' msimu huu baada ya kupona majeraha yaliyomfanya akae nje kwa takribani miezi miwili mwishoni mwa msimu uliopita