Jana Yanga iliendeleza ubabe dhidi ya watani zao Simba, Wananchi wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Ulikuwa mchezo wa rekodi kwa kocha Miguel Gamondi ambaye tangu ajiunge na Yanga hajawahi kupoteza mchezo wowote dhidi ya Simba ndani ya dakika 90
Ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Gamondi ambaye amewafunga makocha watatu wa Simba
Alianza na Robertinho Oliveira ambaye kipigo cha mabao 5-1 kilitosha kumfanya atimuliwe na Simba huku nafasi yake ikichukuliwa na Abdelhak Benchikha ambaye pia akakutana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Gamondi
Fadlu Davies amejiunga na Simba msimu huu nae amekaribishwa na kipigo cha bao 1-0 jana katika mchezo ambao pengine Yanga walistahili kupata ushindi mnono zaidi kama sio makosa ya waamuzi
Aidha Maxi Nzengeli ameingia kwenye rekodi ya wachezaji waliofunga mabao mengi katika mechi za dabi, nae akifikisha mabao matatu kama ilivyo kwa Stephane Aziz Ki
Katika mchi tatu zilizopita dhidi ya Simba, Yanga imepachika mabao 8 huku watani zao wakifunga mabao 2 tu