Hakuna underdog kwenye derby - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Aug 2024
Hakuna underdog kwenye derby - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema amekiandaa kikosi chake kikamilifu kukabiliana na Simba katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Benjamn Mkapa

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi alisema mchezo wa siku zote hauna underdog hivyo watakwenda kucheza kwa tahadhari kubwa wakifahamu huu ni mchezo wa mtoano

Aidha Gamondi amesema hana taarifa za kutosha kuhusu wapinzani wake Simba ambao wana wachezaji wengi wapya lakini anafahamu mpira ni mchezo wa wazi na ameiandaa timu yake kukabiliana nao katika mazingira yoyote

"Yaliyopita yamepita, sipendelei kufuatilia sana yaliyopita, huu ni msimu mpya hata wapinzani wetu pia wamebadilika kila kitu kimebadilika, wacha tuone kesho kitatokea nini"

"Tupo imara kiakili na kimwili, tumejianda vya kutosha hakuna tunachohofia, sijapata wasaa mzuri wa kuwatazama wapinzani kwani mechi zake nyingi hazikuoneshwa, lakini hiyo sio changamoto kubwa kwani naanda timu yangu kwa asilimia 75, asilimia 25 ndio natumia kumchunguza mpinzani"

"Hakuna siri kwenye mpira kila kitu lazima kiwe hadharani, kesho ni siku muhimu sana kwani ni mechi ya mtoano, hatupaswi kufanya makosa tunapaswa kuwa makini kwenye kila idara ili kupata matokeo mazuri, naamini mashabiki wetu watajitokeza kwa wingi kwa lengo la kutupa hamasa"

"Naheshimu sana wapinzani wote ninaokutana nao, kesho ni mchezo wa derby hakuna underdog kwenye mchezo huo kwani ni mchezo maalumu sana, najua mpinzani wetu ana timu mpya, wachezaji wapya, wote kwa pamoja watachukua fursa hii kuonesha ubora wao. Kimsingi mchezo huu mizani ipo sawa kwa pande zote 50/50, ni muhimu sana kuendea mchezo huu kwa umakini mkubwa," alisema Gamondi

Nae mlinda lango Aboubakar Khomein amesema Yanga imejiandaa na mchezo huo kikamilifu, malengo ni kuibuka na ushindi

"Tumejiandaa vizuri sana na tuko tayari, wachezaji wana ari na wote tunawahakikishia kuwa wachezaji tunakwenda kupambana, naamini kesho tutafanya vizuri," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’