Achana na burudani ambayo Wananchi waliipata uwanjani jana katika kilele cha Wiki ya Mwananchi pale dimba la Benjamin Mkapa
Kuna tukio la aina yake ambalo bila shaka litaingia katika vitabu vya kumbukumbu baada ya Yanga kujaza viwanja viwili
Licha ya kumaliza tiketi siku mbili kabla ya Tamasha, mashabiki wengi walibaki nje ya uwanja wa Benjamin Mkapa hali iliyopelekea kufungwa 'krini' kubwa katika uwanja wa Uhuru ili kuwapa fursa mashabiki waliokosa nafasi dimba la Mkapa washuhudie tukio hilo
Umati uliokuwa dimba la Uhuru ukichanganya na wale waliokuwa dimba la Mkapa, pengine ni zaidi ya Wananchi 80,000 walioingia katika viwanja hivyo
Kilichotokea jana ni ujumbe kwa waliokuwa wanabeza ushiriki wa Wananchi katika Tamasha hilo, Yanga imeendelea kudhihirisha ukubwa wake na bila shaka mjadala wa timu ipi ina mashabiki wengi hauna maana tena..!