Mzize uhakika kikosi cha Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Aug 2024
Mzize uhakika kikosi cha Gamondi

Baada ya usajili wa washambuliaji Jean Baleke na Prince Dube, ilionekana kama chipukizi Clement Mzize atakuwa na wakati mgumu kupenya katika kikosi cha kwanza cha kocha Miguel Gamondi

Lakini kinyume na walivyotabiri wengi, Mzize amekuwa na mwanzo mzuri akianza katika mechi zote tatu za pre-season ambazo Yanga ilicheza Afrika Kusini

Katika mechi hizo, Mzize alifunga moja ya mabao ya Yanga kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs na Wananchi kubeba Toyota Cup

Mzize alikuwa miongoni mwa wachezaji walion'gara katika mchezo dhidi ya Chiefs ambapo uwezo wake uliwashangaza hata mashabiki wa Chiefs ambao wamemtaja sana katika mjadala yao kwenye mitandao ya kijamii

Gamondi ameweka wazi kuwa Mzize ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi chake na ataendelea kumpa nafasi

Akizungumza akiwa jijini Dar es Salaam baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini, Gamondi alieleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na Mzize hasa katika mchezo dhidi ya Chiefs

"Mzize alikuwa na mechi nzuri dhidi ya Kaizer Chiefs, naamini atafanya makubwa zaidi msimu ujao, ameonyesha uwezo mkubwa, amekuwa na kasi na utulivu golini, ameendelea kukomaa naamini kama ataendelea kujituma atakuwa mchezaji muhimu sio kwa Yanga tu bali hata timu ya Taifa," alisema Gamondi

Mzize anapata nafasi ya kucheza mbele ya safu bora ya ushambuliaji ya Yanga inayoundwa na Dube, Baleke na Kennedy Musonda ambaye alichelewa kujiunga na wenzake kwenye pre-season kutokana na matatizo ya kifamilia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
26m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
31m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’