Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendelea kununua tiketi kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi August 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kamwe amesema dhamira ya Yanga ni kuona mwaka huu tiketi za Wiki ya Mwananchi zinamalizika mapema huku akiwaahidi Wananchi watashuhudia burudani ya aina yake
Aidha Kamwe amedokeza pia kutakuwa na sapraizi kubwa kwa ajili yao kutoka kwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said
"Mtoko wa kila Mwananchi ni Jumapili pale uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia burudani ya Taifa. Hili sio jambo la kukosa, muda wa kununua tiketi ni huu dalili zinaonkana tiketi zitamalizika mapema"
"Jumapili kutakuwa burudani kutoka kwa wasanii wakubwa, hivi karibuni tutawatambulisha wasanii wote watakaotumuiza siku hiyo"
"Lakini pia kutakuwa na sapraizi kubwa, kuna jambo liko jikoni linapikwa, wahi mapema kwa Mkapa Jumapili ukapate kufahamu," alisema Kamwe
Juzi wakati Yanga ikirejea kutoka Afrika Kusini Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alidokeza pengine wanaweza kuongeza mtu kabla ya dirisha la ndani la usajili kufungwa
Dirisha la usajili la ndani ambalo lilifunguliwa Juni 15, litafungwa August 15 2024