Klabu ya Yanga leo imetangaza kuzindua wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake ni August 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na urejeo wa Haji Manara ambaye anaungana na Ali Kamwe katika kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kamwe amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Yanga kwa kipindi cha miaka mingine miwili
Akitangaza ratiba ya wiki ya Mwananchi, Kamwe amesema kikosi cha Yanga kitawasili Alfajiri ya kesho Jumanne ambapo amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuipoikea timu na kufurahia taji walilotwaa Afrika Kusini
Kesho Jumanne Yanga itatangaza mdhamini wa Wiki ya Mwananchi ambapo siku ya Jumatano itakuwa maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika Hospitali mbalimbali
Alhamisi kutakuwa na zoezi la kuchangisha damu pamoja na matukio ya hamasa ambayo yataanzia Mbagala, Zakhiem
Ijumaa Yanga itafanya dua ya Kitaifa kwa ajili ya kuiombea Yanga, wachezaji, viongozi na wale wote waliotangulia mbele ya hakhi
Jumamosi Makao Makuu ya Yanga kutakuwa na jogging sambamba na ul utaratibu wa supu utafanyika Jangwani takribani ng'ombe 20 wameandaliwa kwa ajili ya zoezi hilo
Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu yake, Manara ameitangaza Red Arrows kutoka Zambia kuwa ndio klabu itakayochuana na Yanga katika kilele cha wiki ya Mwananchi August 04
Red Arrows ni mabingwa wa michuano ya CECAFA Kagame Cup iliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es salaam
Manara amewataka mashabiki wa Yanga kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kilele cha wiki ya Mwananchi ili kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga imejipanga kufanya hamasa kubwa ili kuhakikisha Wiki ya Mwananchi 2024 inakwenda kuwa tukio bora zaidi la burudani