Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo anakwenda kuikabili Kaizer Chiefs akiwa na kikosi chake kamili
Kiungo Pacome Zouzoua ambaye alikosa mechi mbili zilizopita kutokana na matatizo ya kifamilia, amerejea na bila shaka Wananchi leo wanaweza kumshuhudia katika mchezo dhidi ya Chiefs
Pamoja na kuwa ni mechi ya kirafiki, lakini bila shaka Gamondi leo atatumia timu yake bora zaidi ili kuhakikisha Yanga inaibuka na ushindi na kubeba taji la Totyota ugenini
Itakuwa heshima kubwa kwa Yanga kubeba taji hilo mbele ya mashabiki 46,000 wa Kaizer Chiefs ambao wataujaza uwanja wa Toyota Bloemfontien
Wananchi wanasubiri kuona Gamondi ataingiaje leo? hasa ikizingatiwa wachezaji wote wako tayari
Pengine anaweza kuanza na kikosi alichokitumia katika kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya TS Galaxy ambao Yanga ilishinda bao 1-0
Diarra aliingia langoni wakati walinzi wa pembeni walikuwa Yao Kouassi na Nickson Kibabage
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto na Ibrahim Bacca walizima safu ya ulinzi kati huku Khalid Aucho na Maxi Nzengeli walicheza eneo la kiungo cha chini
Hata hivyo Maxi alikuwa na majukumu ambayo Mudathir Yahya huyafanya akipanda na kushuka
Clatous Chama alishambulia kutoka upande wa kulia huku Duke Abuya akitokea kushoto, wakati Aziz Ki akitumika katika eneo lake la siku zote namba 10 na Dube kucheza kama mshambuliaji
Alikuwa Dube aliyefunga bao pekee la Yanga katika mchezo huo wa kuhitimisha Mpulanga Premier's International Cup
Nyota wapya wameleta ushindani na pengine wanaweza kupangua kikosi cha kwanza kilichozoeleka msimu uliopita
Dube, Jean Baleke, Chama, Duke, Andambwile, Boka wote wanataka nafasi katika kikosi cha kwanza
Kikoski kitakachoanza leo pengine kitatoa taswira ya aina ya kikosi ambacho Gamondi ataanza nacho msimu huu