Mapema leo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alihudhuria hafla maalum jijini Johannesburg katika Uwanja wa FNB iliyoandaliwa na kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns, Pitso Mosimane
Hafla hiyo ilikuwa kwa ajili ya kupokea shahada ya heshima ya uzamivu HONORARY DOCTORATE (PhD) kutoka chuo kikuu cha Johannesburg katika kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika
Wengi wanakumbuka Mosimane aliwahi kuja nchini mwaka 2022 kwa mwaliko wa Yanga ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki program za maendeleo ya soka la vijana
Ujio wake ulitoa hamasa kubwa kwa Yanga na ndio msimu ambao Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)





ADVERTISE HERE