TP Mazembe yamruhusu Baleke kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2024
TP Mazembe yamruhusu Baleke kutua Yanga

Sasa ni suala la muda klabu ya Yanga itamaliza sintofahamu kuhusu usajili wa mshambuliaji Jean Baleke ambaye ametua kwa Wananchi kwa mkopo wa msimu mzima

Wakati juzi Baleke anaitumikia na kuifungia Yanga bao katika mchezo dhidi ya Ausburg, mabosi wa Yanga na Mazembe walikuwa wakikamilisha taratibu za nyota huyo kujiunga na Yanga akiwa ametoka kuitumikia Al Ittihad ya Tripoli, Libya

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na TP Mazembe katika tovuti yao, wameidhinisha Baleke kuitumikia Yanga kwa mkopo wa msimu mzima

"Miezi sita baada ya kuondoka Tanzania, Jean Othos BALEKE atarejea huko, akiwa na rangi tofauti. Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye bado ana mkataba na TP Mazembe, ametolewa kwa mkopo tena lakini kwa Young Africans"

"Baada ya msimu mmoja na nusu kukaa Simba SC, BALEKE alienda kwa mkopo Libya, Al Ittihad ya Tripoli. Uongozi wa TPM ulikubali masharti ya mkopo wa mchezaji huyo kwa ajili ya Young Africans," ilibainisha taarifa ya TPM

Licha ya kuonekana viunga vya Avic Town tangu mwanzoni mwa mwezi huu, Yanga haikuwa imemtambulisha rasmi Baleke kwa kuwa ilikuwa katika mchakato wa kukamilisha usajili

Ni wazi sasa wananchi wameunasa mtambo huo wa mabao, August 08 atakuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’