Wachezaji Yanga waahidi ushindi Ethiopia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2018
Wachezaji Yanga waahidi ushindi Ethiopia
Wachezaji wa Yanga wameahidi kupambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mechi ya marudiano ya hatua ya mtoano ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Wolaitta Dicha FC itakayofanyika leo mjini Awassa, Ethiopia.

Wawakilishi hao pekee wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kimataifa wanaingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0, hivyo wanahitaji sare au ushindi wowote ili wasonge mbele.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" amesema kuwa mechi ya leo ni muhimu kwao kwa sababu wanahitaji kuingia katika hatua ya makundi na vile vile kupata fedha zinazotolewa baada ya kufika hatua hiyo.

Cannavaro amesema pia wanatarajia kukutana na changamoto kutoka kwa wapinzani wao lakini akitamba kuwa leo kikosi chao kitakuwa kamili baada ya baadhi ya nyota waliokosekana katika mechi ya kwanza akiwamo straika, Obrey Chirwa, kurejea.

"Mawazo yetu yako katika mechi hii ya kimataifa, ni muhimu sasa kuliko kitu kingine kwa wakati huu, tukirejea nyumbani ndiyo tutaanza kuifikiria Simba na vita ya Ligi Kuu kwa ujumla," amesema Nadir.

Naye Meneja wa Yanga,Hafidh Saleh, amesema kuwa wanamshukuru Mungu wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanachosubiri ni muda ufike

"Maandalizi yako vizuri na kila mchezaji hapa anawaza ushindi na kuvuka hatua hii tuliyopo," alisema meneja huyo.

Hii ni nafasi nyingine kwa Yanga kutinga hatua ya makundi katika michuano ya pili kwa ukubwa ngazi ya vilabu baada ya ile ya ligi ya Mabingwa.

>Mara ya mwisho Yanga kutinga hatua hiyo ilikuwa ni mwaka 2016 ilipokuwa chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm na ilikuwa kundi moja na TP Mazembe, MC Alger na Medeama FC ya Ghana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
58m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’