Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imekubali ombi la Yanga na kutoa siku 14 za mapitio ya kesi inayohusu Bodi ya Wadhamini ya klabu hiyo dhidi ya Juma Magoma na wenzake
Kupitia Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga Ndg. Simon Patrick kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari Julai 17, alibainisha kuwa wataiomba Mahakama kuwapa muda wa mapitio ya kesi hiyo
"Klabu imeomba Mahakama isogeze muda wa Klabu kufanya mapitio ha kesi kwani klabu haikuwahi kushiriki kwenye kesi hiyo, " alisema Simon
Taarifa ya RPM R.S Mushi inasema ombi la Yanga limekubaliwa na Mahakama hivyo Klabu ya Yanga imepewa siku 14 za mapitio ya kesi hiyo
Ni wazi sasa Yanga itakuwa na nafasi ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa August 02 2023 na kuwasilisha hoja zake pamoja na ushahidi juu ya udanganyifu uliofanyika