Bado Yanga haijafunga usajili wake lakini pengine mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii, michakato yote itakuwa imekamilika
Dirisha la usajili la CAF kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) na kombe la Shirikisho (CAF CC) linatarajiwa kufungwa Jumamosi, Julai 20
Katika dirisha hili Yanga imeongeza wachezaji sita ambao ni Aboubakar Khomein, Chadrak Boka, Aziz Andambwile, Duke Abuya, Clatous Chama na Prince Dube
Mchezaji mwingine wa kigeni anayesubiri utambulisho ni mshambuliaji Jean Beleke huku kukiwa na tetesi kuwa Yanga itaongeza beki mwingine wa kati akitajwa Abdulmajid Mangalu kutoka Singida FG
Aidha bado Yanga inajadiliana na beki Gift Fred ambaye huenda akatolewa kwa mkopo na nafasi yake kuchukuliwa na Baleke
Wachezaji wanne wa kigeni ambao usajili wao umetangazwa tayari wamechukua nafasi za Augustine Okrah, Joyce Lomalisa, Joseph Guede na Skudu
Yanga pia imeachana na nyota wengine wa ndani Zawadi Mauya na Metacha Mnata ambao mikataba yao imemalizika