Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anaendelea kukisuka kikosi chake ambapo jioni ya leo program za mazoezi ziliendelea Avic Town
Maandalizi yamepamba moto Avic Town kwani kwa kulingana na ratiba ya pre-season, hakuna muda wa kupoteza kwa Gamondi na vijana wake
Wiki ijayo huenda Yanga ikasafiri Afrika Kusini kushiriki Mpumalanga Premier International Cup ambapo Wananchi wamepangwa kuchuana na Augusburg kutoka Bundesliga Julai 20
Baada ya mchezo huo Yanga itaendelea kusalia Afrika Kusini ikiendelea na pre-season hadi Julai 28 watakapochuana na Kaizer Chiefs katika Toyota Cup
Tukio la Wiki ya Mwananchi litafuatia ambapo shamrashamra kuelekea wiki hiyo itakayohitimishwa uwanja wa Benjamin Mkapa August 04, zitaanza mapema Julai 28
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2024/25 utazinduliwa August 08 kwa mechi za nusu fainali Ngao ya Jamii Yanga ikitarajiwa kuumana na watani zao Simba
Mshambuliaji Jean Baleke ameendelea kujifua na Yanga Avic Town akisubiri utambulisho wake rasmi