Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwanja vyenye sifa ya kutumika katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuanza mwezi August
Kulingana na orodha iliyotolewa, Burundi haina kiwanja chenye sifa ya kutumika katika michuano hiyo msimu huu
CAF imeagiza timu ambazo nchi zao hazina viwanja vilivyokidhi vigezo wanapaswa kucheza mechi zao katika nchi za karibu ambazo zina viwanja vilivyokidhi vigezo
Tanzania ina viwili ambavyo ni Azam Complex na Benjamin Mkapa. Rwanda pia ikiwa na viwanja viwili vya Amahoro na Pele Stadium
Msimu uliopita timu za Burundi zilitumia uwanja wa Azam Complex huku timu yao ya Taifa ikitumia uwanja wa Benjamin Mkapa
Hivyo kuna uwezekano mkubwa Vital'o wataleta mchezo wao dhidi ya Yanga katika uwanja wa Azam Complex