Kwao kama kwetu inahamia Burundi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2024
Kwao kama kwetu inahamia Burundi

Kile ambacho Yanga walifanya kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu uliopita walipokwenda Rwanda kucheza na Al Merrikh, wamepanga kurudia tena watakapokwenda Burundi kumenyana na Vital'o katika hatua ya awali ya michuano hiyo msimu huu

Yanga itachuana na Vital'o August 17-18 nchini Burundi na mechi ya marudiano kupigwa wiki moja baadae jijini Dar es salaam

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema watafanya kampeni kubwa kuhakikisha mashabiki wanakwenda kwa wingi Burundi kama walivyofanya msimu uliopita walipokwenda Rwanda

"Droo tumeiona na tumefurahi sana kwani tutahakikisha tunakwenda kuweka rekodi Burundi kama tulivyofanya Rwanda msimu uliopita tulipokwenda kucheza na Al Merrikh"

"Maandalizi yetu yanaendelea vyema Avic Town, huu ni msimu mwingine ambao tumeweka malengo ya kufanya vizuri zaidi. Ni mechi za mtoano ambazo haupaswi kumdharau mpinzani wako"

"Akili yetu sasa inaziwaza dakika 180 hizi dhidi ya Vital'o, tukishamaliza ndipo tutaanza kuangalia mchezo unaofuata utakuwaje," alisema Kamwe

Kama Yanga itavuka hatua ya awali, raundi ya kwanza itachuana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Sports ya Ethiopia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’