Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Joseph Guede anatarajiwa kujiunga na klabu ya Singida Black Stars (zamani Ihefu Fc), imefahamika
Guede aliitumikia Yanga kwa miezi sita akitua katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita
Hata hivyo uongozi wa Yanga uliamua kutomuongezea mkataba mshambuliaji huyo aliyepachika mabao 11 katika mashindano yote
Guede ataendelea kuonekana ligi kuu ya NBC lakini sasa akiwa Singida
Wananchi wamesajili mshambuliaji mbadala wake ambaye anasubiri kutambulishwa tetesi zikiangukia kwa Jean Balake
Baleke anatarajiwa kujiunga na Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea TP Mazembe
ADVERTISE HERE