Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anaamini kikosi chake kitakuwa bora zaidi kutokana na usajili uliofanyika katika dirisha hili
Gamondi tayari amerejea nchini ambapo jana alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wake, leo anatarajiwa kuongoza mazoezi yatakayofanyika Avic Town
Pamoja na kusifia aina ya usajili uliofanyika, Gamondi amesema atakuwa na wakati mzuri wa kuwatumia wachezaji wote kwa kuzingatia utayari wao na aina ya mechi zitakazokuwa mbele yao
"Niwapongeze viongozi kwa usajili uliofanyika, tulihitaji wachezaji wachache muhimu kwa ajili ya kuboresha maeneo ambayo tulikuwa na changamoto"
"Nina matumaini makubwa na hawa wageni lakini inapaswa tuwape muda wa kuzoea mazingira pamoja na kufahamu mbinu zetu"
"Tutashiriki mashindano mengi msimu huu unaokuja hivyo ni jambo jema kuwa na kikosi kipana ambacho naamini kitatusaidia kufikia malengo tuliyojiwekea"
"Kila mchezaji atapata nafasi kwa kuzingatia utayari wake na kile anachofanya katika kiwanja cha mazoezi," alisema Gamondi
Mpaka sasa Yanga imetambulishwa wachezaji watano wapya ambao ni Aboubakar Khomein, Chadrack Boka, Aziz Andambwile, Clatous Chama na Prince Dube
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema bado hawajamaliza kutambulisha