Mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube, amesema anaamini anaweza kushinda mataji akiwa na mabingwa hao watetezi ligi kuu ya NBC
Nyota huyo ni sehemu ya kikosi kilichoanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa
Dube aliyejiunga na Yanga akitokea Azam FC, amesema lengo lake ni kuona anashinda taji la Ligi Kuu msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa
"Nipo tayari kutoa mchango wangu kwenye timu, naamini naweza kutwaa mataji nikiwa na Yanga. Tumeanza maandalizi na nitahakikisha najituma kwa ajili ya timu," alisema Dube
Dube alikuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Azam kabla ya kuomba kuondoka ndani ya timu hiyo na kujiunga na Yanga
Katika siku mbili ambazo ameshiriki mazoezi na wachezaji wenzake, Dube ameonekana kuwa na furaha wakati wote
Ni wazi alikuwa akisubiri kwa hamu kuanza maisha yake mapya na Yanga