Tutabeba Toyota Cup - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jul 2024
Tutabeba Toyota Cup - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wamepokea kwa furaha mwaliko wa kushiriki michuano ya Toyota Cup itakayofanyika Afrika Kusini Julai 28 kwa mchezo kati ya Kaizer Chiefs dhidi ya Yanga

Kamwe amesema ni heshima kubwa kwa Yanga kupewa mwaliko huo kwani zipo timu nyingine kubwa barani Afrika lakini Chiefs wakaichagua Yanga

Kamwe amesema Yanga itajiandaa vyema na watahakikisha wanashinda taji hilo lililodhaminiwa kampuni ya magari ya Toyota

"Kwanza ni heshima kubwa kwa Yanga kupata mwaliko huu. Kaizer Chiefs wameacha timu zote na kuona Yanga ndio inafaa kushiriki michuano hii inayofanyika kwa mara ya kwanza"

"Tunakwenda kujiandaa vyema na tutawapa Chiefs mechi ya ushindani kwelikweli na lengo letu ni kutwaa taji hilo," alisema Kamwe

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye pia ni Mwenyekiti wa vilabu barani Afrika (ACA), alihudhuria hafla ya uzinduzi wa michuano hiyo ambayo ilifanyika Afrika Kusini jana

Unaweza kusema Yanga ndio iliyoihamasisha Chiefs kuandaa Tamasha hilo ambalo linafanana kabisa na wiki ya Mwananchi

Chiefs walialikwa na Yanga kwenye wiki ya Mwananchi msimu uliopita na kuvutiwa nayo

Mashabiki na Wanachama wa Chiefs watashiriki matukio mbalimbali ya kijamii wiki ya mwisho kuelekea mchezo wa Toyota Cup

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’