Jana kikosi cha Yanga kilianza maandalizi ya pre-season, wachezaji wakifanya vipimo vya afya na jioni kuanza mazoezi ya Gym
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kundi la pili la wachezaji linatarajiwa kuwasili leo ambapo mpaka kufikia Jumatano wachezaji wote watakuwa wameripoti Avic Town
"Tumeanza maandalizi leo (jana) ambapo asubuhi wachezaji walifanyiwa vipimo vya afya Aga Khan Hospital na jioni timu kuanza mazoezi"
"Tunatarajia kundi la pili la wachezaji wengine wataingia leo. Hawa ni wale wachezaji ambao walikuwa na majukumu ya timu za Taifa hivyo walipewa muda zaidi wa mapumziko"
"Mpaka kufikia Jumatano, tunatarajia wachezaji wote watakuwa kambini," alisema Kamwe
Miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajia kuwasili leo ni pamoja na kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye alikuwa mapumziko Ivory Coast
Wengine ni Djigui Diarra, Ibrahim Bacca, Bakari Nondo Mwamnyeto, Kennedy Musonda na Khalid Aucho
Katika hatua nyingine, Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema wameanza pre-season kwa program maalum ya mazoezi mepesi na Gym ambapo siku ya Alhamisi wataanza mazoezi ya uwanjani