Yanga huenda ikatangaza usajili wa kiungo mkabaji wa Singida Fountain Gate Aziz Andambwile
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa nyota huyo tayari yuko jijini Dar es salaam na kama mambo yataenda vyema, atapewa mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa nchi
Yanga ilikuwa na mapendekezo kadhaa ya wachezaji wa ndani kwa ajili ya kuziba nafasi ya Zawadi Mauya ambaye ameruhusiwa kuondoka baada ya mkataba wake kumalizika
Andambwile ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', anaonekana kuwa mbadala sahihi wa Mauya
Andambwile amewahi kucheza soka nje ya nchi katika klabu ya Nyasa Big Bullets mabingwa wa Ligi Kuu ya Malawi
Pia amewahi kuitumikia timu ya Taifa ya Malawi U20 kabla ya kujiunga na Mbeya City na baadae Singida FG ambapo pia alipata wito wa kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania