Baleke ni mtambo wa mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2024
Baleke ni mtambo wa mabao

Chadrak Boka ni mchezaji wa tatu kutambulishwa na Yanga katika dirisha hili akitanguliwa na Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' na Prince Dube

Bado Yanga haijafunga hesabu zake za usajili kwani haijatambulisha golikipa, kiungo mkabaji na mshambuliaji

Utambulisho unaosubiriwa kwa hamu pengine ni ule wa mshambuliaji ambapo Wananchi wakamshuhudia Jean Baleke akirejea tena katika ligi kuu ya NBC

Baleke aliitumikia Simba tangu Januari 2023 hadi Januari mwaka huu alipotimkia Libya

Katika mwaka mmoja aliyoitumikia Simba, Baleke alipachika mabao 16 huku akitoa assist moja katika mechi 18

Alipopelekwa kwa mkopo Libya kunako klabu ya Al ittihad, Baleke pia alipachika mabao sita

Msimu wa 2020/21 Baleke aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya DR Congo mbele ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele

Kwa takwimu zake za misimu minne iliyopita, Baleke ni mshambuliaji ambaye ana uhakika wa kufunga zaidi ya goli 10 kwa msimu

Huyu ni mshambuliaji ambaye hatahitaji muda kuendeleza makali yake katika ligi ya NBC kwani tayari rekodi zinaonyesha amefunga mabao 16 katika muda wa mwaka mmoja aliokuwa hapa nchini kabla ya kutimkia Libya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’