Ngoma, Tambwe tuwape heshima wanayostahili

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
17 Apr 2018
Ngoma, Tambwe tuwape heshima wanayostahili
Kazi ya mchezaji ni kusakata kabumbu. Naamini hakuna mchezaji ambaye atasajiliwa na timu, akawa timamu kiafya halafu akagoma kucheza.

Kutocheza kwa muda mrefu kunaweza kuathiri kiwango cha mchezaji.

Na ndio maana wachezaji ambao huwa hawapati nafasi kwenye timu zao hushinikiza waachwe wajiunge na timu zitakazowapa nafasi ya kucheza.

Nimeanza utangulizi huo ili kuweza kupata kwa kuanzia kulizungumzia sakata la wachezaji Donald Ngoma na Amissi Tamnwe.

Wapo ambao hawaamini wanapoelezwa kuwa ni majeruhi pekee yanayowaweka nje washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

Wawili hawa ni kweli walikuwa wameanza mazoezi, Ngoma alisafiri na kikosi cha Yanga kilipoenda kuikabili Singida United kwenye mchezo wa kombe la FA huku Tambwe akijiunga na kambi waliyokuwa wameweka mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Wolaitta Dicha.



Lakini kwa bahati mbaya wakatonesha majeraha yao hivyo kuwarejesha tena kitandani.

Mara nyingi tumekuwa tukitadharisha juu ya utaratibu wa mashabiki kushinikiza wachezaji waliokuwa majeruhi waanze kuchezeshwa katika michezo migumu.

Huenda presha ya mashabiki iliwafanya watamani kurejea dimbani mapema zaidi licha ya kufahamu kwamba hawakuwa wamepona kikamilifu

Mi nilidhani jambo la msingi hapa ni kuutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha wachezaji hawa wanapona kikamilifu kabla ya kuwaruhusu warejee uwanjani.

Mashabiki ilipaswa wahoji utimamu wa afya za wachezaji waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu wanaporejea dimbani kuliko kuhoji fulani yuko wapi eti kwa kuwa uongozi ulitoa taarifa amepona.

Ifahamike kupona majeraha na kuwa timamu kurudi uwanjani ni mambo mawili tofauti. Mchezaji anaweza kupona majeraha lakini asiwe tayari kuweza kurejea uwanjani.

Kama nilivyosema awali, hakuna mchezaji aliye timamu kiafya ambaye atakubali kukaa nje bila ya kucheza.

Wao wamejaribu mara kadhaa kurejea lakini inaonekana majeraha yao yanahitaji muda na utaalamu zaidi kuweza kupona.

Kimsingi mashabiki tunakosea tunapowashushia lawama sababu hawafanyi makusudi wameumia na hawawezi kucheza katika hali hiyo.

Sote tunafahamu uwezo wa Ngoma na Tambwe wakati walipojiunga na Yanga.

Sasa wanapita kwenye wakati mgumu ni vyema kuwafariji pia tuwe na shukrani kwa kuheshimu mchango wao katika klabu ya Yanga.

Mabao yao kwa kiasi kikubwa yameiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa VPL kwa misimu mitatu mfululizo.

Muhimu watibiwe wapone kama majeraha yao yanatibika, maswala mengine tuuwachie uongozi.

Tukianzisha utaratibu wa kuwa mchezaji akiumia na kukaa nje kwa muda mrefu avunjiwe mkataba wake basi hakuna mchezaji ambaye atakuja kucheza Yanga.

Kwa sababu hakuna mchezaji anayecheza maisha yake yote bila ya kuumia.

Sasa kama tutaanza kuvunja mikataba yao eti kwa kuwa wamekaa nje kwa muda mrefu basi tufahamu tutakuwa tumewafungia milango wachezaji wengi wazuri.

Kuna mchezaji klabu ya Arsenal anaitwa Santi Cazorla, huyu ni majeruhi mwaka wa pili huu, lakini klabu ya Arsenal haikumtupa, imeendelea kumhudumia.

Huko Ulaya ni jambo la kawaida kwa mchezaji kuumia na kukaa nje hadi mwaka mzima. Wao wanaheshimu mikataba walioingia na wachezaji.

Uongozi wa Yanga umeendelea kuwahudumia wachezaji hao sababu ni jukumu lao. Sasa watahudumiwa na nani wakati Yanga ndio muajiri wao?

Mashabiki tunapaswa tujifunze, tusiwe wepesi wa kufurahi mambo yanapokwenda vizuri lakini pia tusiwe wepesi kulaumu mambo yanapokwenda kombo.

Hii Yanga ni timu yetu, tuisaidie pale inapokwama. Sio vizuri kulaumu viongozi na wachezaji bila sababu za msingi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’