Mapema leo Yanga ilithibitisha kuachana na kiungo mshambuliaji Augustine Okrah ikiwa ni miezi sita tu tangu alipojiunga na mabingwa hao wa nchi akitokea Benchem United ya Ghana
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi hakupendezwa na winga huyo mwenye kasi kwa kuwa hakufit katika mfumo wake
Aidha changamoto za nje ya uwanja pia zinatajwa kuchangia kwa Mghana huo kuondoka mapema
Taarifa za Okrah 'kutemwa' zilivuja baada ya msimu uliopita kufika tamati, Okrah mwenyewe akizitoa kupitia waandishi wa habari huko Ghana
Yanga inatarajiwa 'kushusha' winga mwingine wa kuchukua nafasi yake
ADVERTISE HERE