Droo ya makundi ya michuano ya klabu Afrika Mashariki na Kati maarufu CECAFA Kagame Cup ilifanyika jana ambapo michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Julai 06 jijini Dar es salaam
Klabu za Coastal Union na Singida Black Stars ndizo zitakazoshiriki kwa upande wa Tanzania Bara baada ya Yanga, Azam na Simba kujiondoa katika michuano hiyo
Sababu ya Yanga kujitoa katika michuano hiyo ni kutokana na ratiba kuingiliana na muda wa maandalizi ya pre-season
Ratiba hiyo haikuzingatia program za timu shiriki kwani ni wazi hata timu zilizokubali kushiriki hazitakuwa na muda wa kufanya maandalizi jambo ambalo linaweza kuwasababishia changamoto wachezaji kwani wengi wanatoka kwenye mapumziko
Yanga iko katika maandalizi ya pre-season ambapo kikosi kinatarajiwa kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi hayo