Jana usiku Yanga ilithibitisha kumuongeza mkataba kiraka Farid Mussa ambaye ataendelea kubaki Jangwani hadi mwaka 2026
Farid amekuwa Mwanafamilia wa Yanga tangu mwaka 2020, kwa mara nyingine, huduma yake imeendelea kuhitajika
Farid ni aina ya wachezaji ambao unaweza usione mchango wake lakini makocha wengi hupendelea kuwa nao katika timu zao
Alikuwa ni Kocha Nasreddine Nabi aliyefichua uwezo wa Farid kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani
Nabi alimtumia Farid katika safu ya ulinzi upande wa kushoto, winga zote na hata nafasi zote za kiungo
Hata Miguel Gamondi msimu uliopita aliendelea kumtumia Farid katika maeneo tofauti kwa kuzingatia mahitaji ya mechi
Gamondi ndiye aliyependekeza kiraka huyo aongezwe mkataba baada ya kuridhishwa na uwezo wake
Kulikuwa na tetesi klabu za Azam Fc na Simba zilikuwa zikimnyemelea lakini haikuwezekana kwa sababu bado anahitajika Jangwani