Baada ya kukamilisha usajili wa Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka, unaweza kusema Rais wa Yanga Injinia Hersi Said anakwenda kuunda 'dream team'
Unapozungumzia wachezaji bora katika ligi kuu ya NBC, basi mpaka muda huu wote wako Yanga. Hii Yanga inayoundwa na Hersi ni timu ya kufikirika, ni mara chache sana timu ya aina hii hutokea
Ni kwenye 'playstation' tu kwa wale wanaocheza 'game' za FIFA na eFootball huweza kuunda timu za ndoto zao kama alivyofanya Hersi kwa Yanga
Bado kazi hajamalizika! kwani kuna wengine wanasubiri kutambulishwa akiwemo Mwana Mfalme ambaye usajili wake unakwenda kukamilisha 'Dream Team'
Hiki kikosi cha Yanga cha msimu huu kinaweza kikaingia katika rekodi za klabu na pengine kitazungumzwa kwa miaka mingi ijayo
Hili pigo walilopigwa watani leo, inaweza kuwa KO ya mapeeeema kuelekea msimu ujao
Kwani kabla ya kupigwa na kitu kizito asubuhi ya leo, walikuwa na matumaini Chama angesalia!