Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya vijana wa Safari Champions umemalizika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1
Yanga ikianza na nyota wachache wa kikosi cha kwanza, ilitawala mchezo huo na kuwapa darasa huru vijana wa Safari Champions waliokuwa wakinolewa na nyota wa zamani wa Yanga Sekilojo Chambua na Mrisho Ngasa
Kinda Shekhan Khamis ni miongoni mwa waliofunga mabao ya Yanga huku mengine yalifungwa na Omary Mfaume, Prosper na Hussein wote kutoka Yanga U20
Katika mchezo huo pia alionekana kiungo Hassan Ssenyonjo kutoka klabu ya Wakiso Giants ya Uganda
ADVERTISE HERE