Ni wazi Tamasha la Wiki ya Mwananchi kuelekea msimu ujao litakuwa la aina yake na pengine litakuwa Tamasha la kwanza ambalo Yanga wanaweza kumaliza tiketi mapema kuliko wakati mwingine wowote
Baada ya mafanikio ya timu yao katika misimu mitatu mfululizo, pamoja na aina ya usajili ambao Yanga wamefanya, Wananchi wako tayari kwa tamasha hili na linakwenda kuvunja rekodi
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kuanzia Julai 1 wataanza kutangaza taarifa za maboresho ya kikosi na pale watakapokamilisha zoezi hilo, mipango ya kuelekea wiki ya Mwananchi itawekwa wazi
Aidha Yanga itaondoka nchini mwanzoni mwa Julai kwenda kuweka kambi nje ya nchi, na pale watakaporejea ni katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi
Baada ya kukosekana kwa misimu miwili ya wiki ya Mwananchi kutokana na kifungo, Haji Manara 'Buggati' amemaliza kifungo na atakuwepo katika Tamasha linalofuata
Manara ametamba kuwa tayari ameanza kufanya mazoezi kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wapya
Aidha kuna taarifa kuwa mabosi wa Yanga huenda wakaialika klabu ya Mamelodi Sundowns katika Tamasha hilo
Yanga bado haijamalizana na Sundowns kutokana na kile kilichotokea katika ligi ya mabingwa msimu uliopita