Jambo la uhakika ni kuwa kuna bango la usajli linaandaliwa na litakaa karibu kabisa na yalipo Makao Makuu ya klabu moja marufu hapo mitaa ya Kariakoo
Hii ni ahadi iliyotolewa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na kila mara msemaji wa Yanga Ali Kamwe ameiwekea msisitizo
Tetesi nyingi zimeelekezwa kwa kiungo wa Simba Clatous Chama, lakini je ni yeye? majibu ya swali hili yatapatikana baada ya Juni 29
Katika misimu ya karibuni Chama amehusishwa kusajiliwa na Yanga lakini mwishoni aliendelea kuwatumikia waajiri wake, Simba
Wapo wanaoamini ni mbinu ambayo Yanga wamekuwa wakiitumia 'kuwapigisha short' watani zao kila dirisha la usajili linapofika
Ilifanyika hivyo kwa Kibu Denis ambaye baada ya mkataba wake kuisha zikavuma tetesi kuwa Yanga wako mbioni kumsajili jambo lililopelekea Simba wamuongezee dau ili kumshawishi asaini mkataba mpya
Baadae Msemaji wa Yanga Kamwe akakanusha kuwa Kibu hakuwa mchezaji waliolenga kumuweka kwenye bango, mchezaji huyo yupo na atafahamika wakati utakapofika
Mara kadhaa Injinia Hersi ameweka wazi kuwa Chama ni mmoja wa wachezaji bora aliowahi kuwashuhudia katika ligi ya Tanzania Bara na iwapo atapata nafasi ya kumsajili hatasita kufanya hivyo
Je wakati huu Yanga imefanya kweli au ndio yale yale ya misimu iliyopita....?
Tusubiri.....!