Hersi, Dube watupia timu Job ikishinda 6-2

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2024
Hersi, Dube watupia timu Job ikishinda 6-2

Tamasha la Wape Tabasamu limefana mkoani Morogoro ambapo mastaa mbalimbali wa soka, viongozi na wasanii walishiriki kuwaunga mkono Kibwana Shomari na Dickson Job walioandaa Tamasha hilo kwa ajili ya kurejesha kwa jamii

Timu Job wakaibuka na ushindi wa mabao 6-2 huku Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akifungua akaunti ya mabao kwa upande wa timu Job kwa bao safi la kichwa

Hersi ambaye alicheza kwa takribani dakika 22 aliongoza safu ya ushambuliaji ya timu Job sambamba na Prince Dube ambaye pia alifunga moja ya mabao ya timu Job

Mabao mengine yalifungwa na Said Ndemla, George Mpole, Samson Mbangula na Edwin Balua huku mabao yote ya timu Kibwana yakifungwa na Saimon Msuva

Ali Kamwe ndiye aliyekuwa kocha wa timu Job huku Hasheem Ibwe akiwa kocha wa timu Kibwana

Katika mchezo huo pia Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Morogoro mjini Mh Aboud walipata dakika chache katika kikosi cha Kibwana

Tamasha hilo lilifikia malengo kwani wakazi wa mkoa wa Morogoro walijitokeza kwa wingi wakiujaza uwanja wa Jamhuri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’