Edna Lema aaga Biashara United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2024
Edna Lema aaga Biashara United

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Biashara United Edna Lema amewaaga waajiri wake hao wa zamani baada ya mkataba wake kumalizika

Lema alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Biashara United lililoiwezesha timu hiyo kucheza play-off ya kupanda ligi kuu dhidi ya Tabora United wakipoteza kwa kufungwa mabao 2-1

"Ulikuwa ni msimu mzuri kwetu na kwangu pia, tulifanya kila kilichokuwa ndani ya uwezo wetu lakini hatukuweza kufikia malengo kwa asilimia 100 yote kwa yote tunashukuru Mungu kwa kuwa yeye ni mjuzi zaidi"

"Niwashukuru Uongozi wa Biashara UTD, Benchi la Ufundi likiongozwa na Aman Josia, wachezaji wote wakiongozwa na Captain Babilas Chitembe kwa wakati wote tuliokuwa pamoja tumeishi kama familia yale mazuri tuyaendeleze na kwa yale mapungufu tusamehane pia"

"Biashara imechangia kunikuza na kuniongezea uzoefu katika kazi yangu ya Ukocha. Niwatakie kila lenye kwa msimu ujao Ni ngumu kusema kwaherini lakini kwa kuwa maisha ya mpira ni mzunguko tutakutana wakati mwingine Asanteni sana Mungu awabariki," aliandika Lema katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Lema anatarajiwa 'kurejea nyumbani' katika kikosi cha Yanga Princess 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’