Yanga bado haijamalizana na aliyekuwa mchezaji wao Lazarus Kambole na hivyo kuendelea kuwa katika kifungo cha kutosajili kutoka kwa Shirikisho la soka Duniani (FIFA)
Kifungo hicho kimepelekea Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuizuia Yanga kusajili hadi pale itakapomalizana na Kambole
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo imebainisha kuwa Yanga ni miongoni mwa timu zilizozuiwa kusajili
Hata hivyo kifungo hicho kitaondolewa mara moja baada ya kumalizana na suala la kambole
Yanga ilikuwa na vifungo viwili kutoka FIFA, ilifanikiwa kumaliza kifungo kimoja huku ikitarajiwa kukamilisha awamu ya mwisho ya malipo ya Kambole
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewatoa hofu mashabiki na wanachama wa Yanga kuwa uongozi wao uko makini na watamaliza changamoto hiyo na timu itasajili