Msimu wa kwanza kwa Kocha Miguel Gamondi akiwa na kikosi cha Yanga umekuwa wa mafanikio makubwa kwake pengine kuliko wakati mwingine wowote katika maiisha yake ya ukocha wa mpira wa miguu
Achana na mafanikio yake ya kutwaa mataji mawili makubwa yaani ligi kuu na kombe la Shirikisho la CRDB, huku pia akiiongoza Yanga kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kusubiri kwa miaka 25
Katika msimu uliopita, Yanga iliweka rekodi ya kupachika mabao mengi katika mashindano yote
Mabao 71 yalifungwa katika ligi kuu ya NBC, mabao 19 yakafungwa kwenye CAF CL, mabao 15 yakafungwa katika michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB
Lakini pia katika kombe la Mapinduzi Yanga ilipachika mabao nane huku mabao mawili yakifungwa kwenye Ngao ya Jamii
Yanga ilipachika mabao 115 katika mashindano yote msimu uliopita. Hii inaweza kuwa ni rekodi kwa Wananchi
