Senzo ampongeza Mtine kwa kazi nzuri Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2024
Senzo ampongeza Mtine kwa kazi nzuri Yanga

Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini amesema mrithi wake Andre Mtine anastahili pongezi kutokana na mafanikio ya timu hiyo

Senzo aliyekuwa CEO wa Yanga kwa kipindi cha msimu mmoja wa 2021-2022, amesema Mtine raia wa Zambia amekuwa kiongozi mwenye maono makubwa ya wakati ujao, jambo ambalo linaleta matunda mazuri klabuni hapo

Senzo aliyasema hayo jan Jumamosi Juni 15, 2024 katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Yanga iliyofanyika Hyatt Regency jijini Dar es Salaam

"Tuipongeze Yanga, tuupongeze uongozi chini ya Rais Hersi Said sambamba na mafanikio waliyokuwa nayo kuipeleka mbele klabu bila ya kumsahau huyu jamaa (Andre Mtine) CEO mwen-zangu tumpongeze naye kwani wamebeba ubingwa mfululizo akiwa sehemu ya watu muhimu sana, ni kitu kizuri," alisema Senzo

Mtine alitangazwa kuwa CEO wa Yanga Septemba 27, 2022 akichukua nafasi ya Senzo aliyeitumikia nafasi hiyo klabuni hapo kuanzia Agosti 2021 hadi Julai 2022

Mzambia huyo tangu awe CEO wa Yanga, timu hiyo imebeba mataji mawili ya Ligi Kuu Bara (2022-2023 na 2023-2024) na Kombe la Shirikisho (FA) mara mbili (2022-2023 na 2023-2024)

Pia Yanga imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 ikipoteza kwa kanuni ya bao la ugenini mbele ya USM Alger baada matokeo ya jumla kuwa sare ya mabao 2-2, huku 2023-2024 ilicheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 25 ilipocheza mara ya mwisho 1998

Senzo wakati akiitumikia Yanga alikuwepo katika mafanikio ya timu hiyo katika kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara 2021-2022 na Kombe la Shirikisho (FA) msimu huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’