Aucho ajipanga kurejea kivingine msimu ujao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2024
Aucho ajipanga kurejea kivingine msimu ujao

Kiungo mkabaji wa Yanga, Khalid Aucho amesema anautumia muda wake wa mapumziko kuhakikisha anarejea kwenye utimamu wa mwili, ili msimu ujao awe fiti na kufanya makubwa Ligi Kuu Bara.

Msimu ulioisha Aucho aliumia goti mechi ya ugenini ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly ya Misri, ambapo alifanyiwa upasuaji mdogo wa goti, kitu kulichomfanya akae nje ya uwanja, ili kuuguza majeraha yake.

"Kipindi Ligi Kuu inachezwa sikupata muda wa kupumzika vizuri, ndio maana nipo makini nisiuchoshe mwili wangu na kuiruhusu akili kuingiza vitu vipya, ili nikirejea kwenye majukumu nakuwa nguvu mpya.

"Ukiona kiwango cha mchezaji kipo juu, huyo anakuwa yupo vizuri kwenye akili yake, anakuwa fiti kimwili, kwani soka halina njia za mkato wala kubahatisha.”

"Ndio maana nikiwa mapumziko napenda kutumia muda mwingi nikiwa na ndugu, jamaa na marafiki, kubadilishana nao mawazo ya kimaisha, hivyo naepuka kuyapa nafasi masuala ya soka, ili nisije nikarejea kazini nikiwa sina ari ya kufanya nzuri,"alisema

Aucho alisema msimu ulioisha haukuwa mzuri kwake, kutokana na kupitia changamoto za majeraha, hivyo anatamani ujao uwe wa kung’ara katika karia yake.

"Ingawa furaha yangu ilikuwa ni kuona Yanga inanyakua mataji na hilo lilifanikiwa, kama mchezaji nilitamani huduma yangu iwe bora, bahati mbaya nikaumia nikashindwa kutimiza ndoto zangu, lakini msimu ujao nina imani utakuwa bora kwangu," alisema Aucho

Aucho alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda kilichocheza mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia 2026 hata hivyo hakutumika katika mechi hizo kutokana na majeraha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’