Yanga kuamua hatma ya ushiriki Kagame Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jun 2024
Yanga kuamua hatma ya ushiriki Kagame Cup

Uongozi wa Yanga unatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusiana na ushiriki wao katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kagame Cup yaliyopangwa kufanyika kuanzia Julai 6 hadi 22, mwaka huu hapa nchini

Mpaka jana Yanga ilikuwa haijathibitisha kushiriki michuano hiyo itakayofanyika kwenye viwanja vya Tanzania Bara na Zanzibar

Awali michuano hiyo ilipangwa kuanza Julai 19 lakini sasa imerejeshwa nyuma Julai 06 kipindi ambacho maandalizi ya msimu mpya wa mashindano yanatarajiwa kuanza

Wachezaji wa Yanga walipewa likizo ya mwezi mmoja na wanatarajiwa kurejea mwanzoni  mwa Julai

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe, amesema uongozi wa klabu hiyo utaweka hadharani uamuzi waliofikia kuhusu mashindano hayo hivi karibuni ili kila mwanachama afahamu mustakabali wao

"Uongozi unajiandaa kutoa tamko la klabu, wanachama na mashabiki watulie, tutatoa tamko letu rasmi kuhusiana na mashindano haya," alisema Kamwe

Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaam, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisema klabu imepata mualiko wa kufanya pre-season katika nchi moja barani Ulaya

Ni wazi ratiba inaweza kuwa changamoto kwa upande wa Yanga kushiriki michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’