Yanga iko mbioni kumuongeza mkataba mshambuliaji Joseph Guede raia wa Ivory Coast
Nyota huyo aliyewahi kutamba na klabu ya FAR Rabat, alisajiliwa na Yanga katika usajili uliopita wa dirisha dogo akisaini mkataba wa miezi sita
Guede amewashawishi mabosi wa Yanga na Kocha Miguel Gamondi baada ya kufanya vizuri katika nusu msimu alioitumikia Yanga
Katika mechi 17 za ligi, Guede alipachika mabao sita huku akitoa pasi mbili za mabao. Pia alipachika mabao matatu katika kombe la Shirikisho na kufunga bao moja katika ligi ya mabingwa
Amefunga mabao 10 katika mashindano yote akihusika katika mabao 12 kwa jumla
ADVERTISE HERE