Klabu ya Yanga jana iliingia makubaliano na Kampuni ya bia nchini (TBL) kucheza mchezo maalum na kikosi cha Safari Champion Juni 29 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
TBL iliendesha mashindano maalum ya kusaka vipaji na kuchagua wachezaji waliounda timu hiyo ya Safari Champion
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Andrew Ntime, amesema makubaliano hayo yatasaidia kuinua vipaji vya vijana ambao watazitumikia timu za Taifa hapo baadaye
"Hii ni fursa ya pekee kwetu kuingia makubaliano na kampuni hii katika kuhakikisha tunaibua vipaji vya vijana ambao hapo baadaye watazitumikia timu za Taifa," alisema Mtime
Meneja wa TBL, Pamela Kikalu, alisema timu hiyo ya Safari Champion ina jumla ya wachezaji 22 ambao wamepatikana katika mikoa minne ya Tanzania Bara, kupitia mchakato wao uliaoanza mwezi Agosti mwaka jana
"Mchakato huu ulianza tangu mwezi Agosti kwa kukusanya vijana zaidi ya 1,000 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ambao tuliwafanyia mchujo na kupata idadi hii," alisema Kikalu
Mbali na Tamasha hilo, vile vile kutakuwa na burudani zitakazotolewa na wasanii Harmonize wa Tanzania pamoja na Koffi Olomide kutoka Kongo.